Welcome



WELCOME
TO THE WORLD OF ENTERTAINMENT AND INTERNATIONAL STARDOM


Tuesday, June 18, 2013

STEPS BONGO MOVIE AWARDS

Kwa muda mrefu sasa tasnia ya filamu TANZANIA imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi,lakini mojawapo ni utoaji wa TUZO katika tasnia hii imekuwa hakuna kabisa ukilinganisha na ukubwa na ukuaji wa tasnia ya FILAMU hapa nchini.
Kampuni kubwa kabisa hapa nchini ya usambazaji wa kazi za wasanii STEPS ENTERTAINMENT imezindua rasmi mwaka huu TUZO za filamu na zitakuwa zikifanyika kila mwaka jamba ambalo wadau na wasanii kwa ujumla wameliongelea kama ni hatua kubwa sana na ukombozi wa wasanii wa maigizo nchini.TUZO hizo zitajulikana kama STEPS BONGO MOVIE AWARDS na kwa mwaka 2012-2013 zimefanyika pale BLUE PEAL ubungo plaza huku zikishuhudiwa na mamia ya watu na mamilioni ya watanzania kupitia TBC1 na CLOUDS TV.
Kwa mwaka huu wametoa vipengele vichache kama,muigizaji bora chipukizi,movie bora ya mwaka,muigizaji bora wa mwaka(mke\mme),tuzo za waliofariki,muongozaji bora,na nyingine nyingi huku wasanii kama JB,VICENT KIGOSI,IRENE UWOYA,STEVEN KANUMBA,ALLY YAKUTI,IRENE PAUL na wenginewo kuwa vinara wa TUZO hizo kwa mwaka huu.



No comments:

Post a Comment