WelcomeWELCOME
TO THE WORLD OF ENTERTAINMENT AND INTERNATIONAL STARDOM


Tuesday, April 8, 2014

MAISHA PLUS

Msimu wa nne wa show ya ukweli MAISHA PLUS unaendelea kuruka TBC1 kila siku jumatatu mpaka jumapili saa nne kamili usiku huku shindano hilo kwa mwaka huu limepewa jina la MAISHA PLUS REKEBISHA.Washiriki wanaendelea kuREKEBISHA  kama kauli mbiu ya shindano inavyosema,tukumbuke mwaka huu nchi nne zimeshiliki na mwisho wa shindano hili kijana mmoja atajinyakulia kitita cha tsh25m na katika MAMA SHUJAA ambayo hivi karibuni wamama mbalimbali wakulima wadogo wadogo wataungana na vijana wa maisha plus kijijini na mmoja wao ataondoka na pembejeo za KILIMO zenye thamani ya tsh10m.

Thursday, April 3, 2014

hayawi hayawi...

Baadhi ya hizi sura zitaonekana sana katika kazi za FILAMU zinazokuja kutoka TRIPLE S INC. hivi karibuni,akiongea na blog hii meneja masoko wa kampuni iyo bwana ISACK JOHN amesema kampuni ya TRIPLE S INC. imejiandaa kikamilifu kuwaletea WATANZANIA burudani kemkem na za kutosha kutoka katika kampuni yao.Bw ISACK JOHN akuishia hapo bali aliwataja baadhi ya wasanii watakaoonekana sana katika FILAMU zao za hivi karibuni kwamba ni JUMA NKWABI,NANCY MANONGI,NANZA MBUJI,CHUCHU HANS,SULEIMAN BARAFU na wengine wengi bila kumsahau mkurugenzi wa kampuni iyo bw STEVEN SANDHU.
Wapenzi wa filamu kaeni tayari...