Welcome



WELCOME
TO THE WORLD OF ENTERTAINMENT AND INTERNATIONAL STARDOM


Wednesday, April 17, 2013

NENO LA MWISHO KUNIAMBIA BI KIDUDE.

Ilikuwa ni muda kidogo tangu nionane na marehemu BI KIDUDE BARAKA. na ilikuwa mwaka jana mwanzoni nilipoenda visiwani ZANZIBAR kuchukua picha na kurekodi moja ya filamu zangu na nakumbuka kazi iyo pia nlishilikishwa pamoja na mkongwe huyo wa musiki wa taarabu na nakumbuka tulifanya kazi ile kama siku tano hivi na tulipomaliza siku ya mwisho tulicheza sana ngoma maana location ya mwisho ya kazi ile ilikuwa kijijini na tulimalizia huko na kufanya sherehe ndogo ya kumaliza kazi,Lakini mwisho kabisa nlijikuta nimekaa pamoja na bibi huyo kibalazani na tulipiga stori nyingi uku tukicheka kwa furaha,lakini ghafla aliniita na kuninongoneza kitu taratibu sikioni kwa sauti ya upole huku akiwa na furaha alinambia "ukiondoka kurudi bara usisahau kuja kunisalimia na kunitembelea nyumbani tena"nlicheka na nikamwambia nitakuja mke wangu.....na baadaye ile sherehe ilimalizika na tukamrudisha mpaka nyumbani kwake,nakumbuka.



Kitu kinachonisikitisha zaidi ni kwamba sikuenda kumuona tena na kila nlipopanga kwenda visiwani ZANZIBAR nlijikuta ratiba zangu zimebana.dah imenisikitisha sana aseee
R.I.P bibi yetu tutakukumbuka milelele ...

No comments:

Post a Comment